Wapalestina washukiwa kuua na kuteka

Polisi wa Israel akiwa West Bank
Maelezo ya picha,

Polisi wa Israel akiwa West Bank

Jeshi la Israel limesema wapalestina wawili wanashukiwa kuhusika katika kuteka na kuua vijana watatu wakiisrael mapema mwezi juni mwaka huu , ambapo walifyatua risasi katika mapambano ya awali huko Gaza na kuuwa watu kwenye oparesheni hiyo.

Msemaji wa jeshi (luteni colonel Peter Lerner) alisema mmoja wa wanaume hao alikufa walipokuwa wanafanya mabadilishano ya risasi na kikosi maalum cha Israeli huko Hebron .

Vyanzo vya jeshi la israeli linaamini kuwa wanaume wengine walikufa pia, lakini wanasubiri taarifa rasmi za uthibitisho.

Ndugu wa kijana mmoja tayari ameshitakiwa kwa kosa la mpango wa kuteka nyara.