Mateka Mrejumani aachiliwa Somalia

Taarifa ziliarifu kuwa mjerumani huyo alitekwa nyara na maharamia miaka mitatu iliyopita
Maelezo ya picha,

Taarifa ziliarifu kuwa mjerumani huyo alitekwa nyara na maharamia miaka mitatu iliyopita

Maafisa wa utawala nchini Somalia, katika jimbo la Puntland, wamethibitisha kuwa mateka mjerumani Michael Scott, ameachiliwa leo.

Naibu kamishna wa jimbo hilo, (Ahmed Muse Noor) amesema kuwa bwana Scott, ambaye ni mwandishi wa habari,alitekwa nyara miaka mitatu iliyopita.

Bado haijulikani ni nani aliyemteka nyara mtu huyo, lakini mwaka 2012, kanda ya video ilitolewa ikitaka kikombozi cha dola milioni 20 ili aweze kuachiliwa.

Kulikuwa na vitisho pia vya kumuuza kwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu ya Al Shabaab.

Duru zilisema kuwa huenda ni maharamia waliomteka nyara mwanamume huyo.

Kuna ripoti kuwa kikombozi cha dola milioni moja na nusu kilitolewa kumnusuru mwanamume huyo lakini serikali bado haijathibitisha madai hayo.