Sera ya kipekee ya Branson kuhusu likizo

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waruhusu wafanyikazi wachukue likizo kila wanapotaka .

Mmiliki wa Kampuni ya Virgini Sir Richard Branson amewaruhusu wafanyi kazi wake kuchukua likizo wakati wowote wanapotaka.

Kwenye mtandao wake Branson ambaye ni mmiliki wa shirika la ndege la Virgin alisema kwamba wafanyikazi wake 170 wanaweza kuchukua likizo wakati wowote wanavyotaka na kwa muda wanaotaka .

Aliongeza pia hakuna haja ya kuuliza ruhusa wakati wanaporejea kazini kwani hata kama hawako kampuni haiwezi kuzama.

Branson alisema kuwa alishawishiwa na binti yake ambaye alisoma kuwa mpango kama huo kwa mtandao wa televisheni ya kampuni ya Netflix.

Milionea huyu alisema ''ni wajibu wa kila mfanyi kazi kuamua lini anajisikia kupumzika na lini anataka kuendelea na kazi.

Wazo langu ni kuwa ikiwa mfanyikazi atahisi yakwamba anastahili kufanya kazi atajitolea asilimia 100% na kuwa hata akiamua kuchukua likizo hakuna hatari ya kampuni kuporomoka '' alisema Branson

''Ukiangalia sheria za likizo nchini Marekani na Uingereza utagundua kuwa ni vigumu sana kubadili chochote wafanyikazi wanashurutishwa kuchukua likizo wakati maalum na kuwa ni mwajiri ndiye anayetoa maagizo lini likizo itachukuliwa'' si haki hivyo

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waruhusu wafanyikazi wachukue likizo kila wanapotaka .

''inapaswa tusistize utendakazi mwafaka wala sio ratiba ya kuingia kazini asubuhi saa tatu na kuondoka saa kumi na moja ''

Blogu hiyo ya Branson ni kionjo tu kitabu chenyewe kitachapishwa hivi karibuni.

Kampuni yake ya Virgin imewaajiri zaidi ya watu 50,000 katika mataifa 50 kote duniani.

Branson alianzisha kampuni hiyo ya Virgin mwaka wa 1970 wakati huo akisafirisha barua na uchukuzi wa bidhaa za wateja hadi sasa inapojishughulisha na mawasiliano uchukuzi na hata sekta ya fedha na uchumi.