FBI yamtambua mpiganaji wa jihad

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mkurugenzi wa FBI nchini Marekani,James Comey

Mkurugenzi wa shirika la upelelezi la marekani FBI, amesema ofisi imemtambua mmoja wa wanamgambo wa Islamic State aliyekua ameuficha uso wake aliyehusika na mauaji ya Waandishi wa habari wa Marekani na mfanyakazi wa shirika la misaada, raia wa Uingereza.

Shirika hilo halijataja jina na uraia wa mtu huyo, lakini serikali ya London imesema anaonekana kuwa muingereza.

James Comey amesema muuaji ametambulika kwa msaada wa washirika wao wa kimataifa.

Mauaji ya kikatili yaliyofanyika dhidi ya James Foley, Steven Sotloff na David Haines yalitolewa kwenye video na kupelekwa kwenye mitandao na wanamgambo hao wa Islamic State na kuchochea mapambano dhidi ya wapiganaji wa Jihad.