Sierra Leone yazidisha karantini nchini

Haki miliki ya picha AP
Image caption Janga la Ebola limetikisa zaidi kanda ya Afrika Magharibi ikiwemo Sierra Leone, Liberia na Guinea

Serikali ya Sierra Leone imeweka wilaya tatu chini ya karantini katika vita vyake dhidi ya Ebola.

Wilaya nyingine tano kati ya 14 na karibu thuluthi moja ya watu nchini humo ambao idadi yao ni milioni moja pia watakuwa chini ya karantini.

Hatua ya serikali inafuata siku tatu za amri ya kutotoka nje ambayo ilimalizika Jumapili.

Rais Ernest Bai Koroma amesema kutangaza karantini katika wilaya hizo, kutasababisha changamoto lakini cha muhimu zaidi ni kunusuru nchi.

Shirika la afya duniani linasema takriban watu elfu tatu wamefariki kutokana na Ebola katika kanda ya Afrika Magharibi huku Sierra Leone, Liberia na Guinea zikiwa baadhi ya nchi zilizoathirika zaidi.

Shirika hilo lilisema kuwa hali nchini Guinea inaoenakana kuwa shwari kidogo ingawa kuna wasiwasi kuhusu kiwango cha maambukizi.