Binzari ya manjano kutibu ubongo?

Image caption Manjano iliyosagwa

Jarida moja liitwalo journal Stem Cell Research and Therapy kwa muujibu wa utafiti wake limegundua kua binzari ya manjano inaouwezo wa kusababisha ubongo kujitibu wenyewe .

Utafiti huo kutoka nchini Ujerumani unaeleza kua kiungo hicho husababisha ukuaji wa seli za mishipa ya fahamu na kutajwa kua kiungo hicho kina uwezo wa kuutibu ubongo.

Wanasayansi wanasema kwamba majaribio kadhaa ya kitabibu yametajwa kufanywa kwa panya ,na kwamba siku za usoni dawa hii inaweza kutumika kuwatibu watu waliopooza mwili na viungo lakini pia wenye ugonjwa wa Alzeima.

Wanasayansi hao wamesema majaribio kadhaa hayanabudi kufanywa ili kuona kama tiba hiyo ina faa kwa binaadamu.

Sindano ya viungo

Haki miliki ya picha THINKSTOCK
Image caption manjano

Watafiti kutoka idara ya Neuroscience na Medicine mjini Julich, nchini Ujerumani wanasema kwamba walimchoma sindano panya na kisha ubongo wake kuchunguzwa .

Sehemu ambazo zinahusika na ubongo, ambazo zina husika na ukuaji wa seli, zilionesha kuchangamka baada ya kudungwa sindano hiyo.

Scientists say the compound may encourage a proliferation of brain cells.

Dokta Laura Phipps mtafiti wa kujitolea katika kituo cha utafiti cha Alzheimer Research UK, amesema kwamba haijawa dhahiri kama utafiti huu mpya utaelekezwa moja kwa moja kwa binaadamu ama uzalishwaji mpya wa seli za binadamu utawafaidia wenye ugonjwa wa Alzheimer .