Mchinjaji wa IS atambuliwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mkurugenzi wa FBI James Comey

Mkurugenzi mkuu wa FBI James Comey amesema kitengo chake kimemtambua mtu ambaye huficha sura yake ambaye ni muuaji,ambaye pia huoneshwa wakati akiwachinja mateka watatu kwenye video inayo nadi wanamgambo wa dola ya kiislam IS.

Pamoja na hayo Bwana Comey amegoma kuutaja uraia wa mtu huyo ama hata kutaja jina lake,ingawa imeshajulikana lafudhi ya mtu huyo kuwa ni mwenye asili ya mji wa London, na Comey amesema kwamba utambuzi wa mtu huyo umefanikishwa kwa msaada mkubwa wa marafiki wa kimataifa.

Muuaji huyo wa waandishi James Foley na Steven Sotloff pamoja na mfanyakazi wa kujitolea David Haines walipigwa picha ya video na kuwekwa kwenye mitandao na wanamgambo hao wa dola ya kiislam na kusaidia kufanya maamuzi juu ya mipango ya wapiganaji wa jihad.