Zimbabwe yanyimwa mkopo na IMF

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Nemboya IMF

Hazina ya fedha duniani IMF imesema kuwa haitatoa fedha zaidi kwa serikali ya Zimbabwe kwa kuwa serikali hiyo ina madeni chungu nzima.

Kundi la wataalam wa hazina hiyo barani afrika liko mjini Harare kukamilisha mpango wa kuisadia serikali kuimarisha uchumi wake huku maelezo ya mpango huo yakitarajiwa kutolewa wiki ijayo.

Naibu mkurugenzi wa hazina hiyo anayesimamia Afrika Domenico Fanniza ,ameiambia BBC kwamba utoaji wa mikopo mipya haupo katika mpango wao kwa sasa..

Bwana Fanizza pia alionyesha wasiwasi wake kuhusu hatua ya serikali kutumia robo tatu ya fedha za kodi kulipa mishahara ya takriban wafanyikazi laki mbili na nusu wa serikali.