USA:Kampeni ya angani yasambaratisha IS

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jenerali Martin Dempsey Kushoto.

Mkuu wa jeshi nchini Marekani Jenerali Martin Dempsey amesema kuwa mashambulizi ya angani dhidi ya kundi la Islamic State yameliharibu kundi hilo,lakini akaonya kuwa kampeni hiyo ya angani pekee haiwezi kuliangamiza kundi hilo.

Amewaambia waandishi habari kwamba kampeni ya nchi kavu dhidi ya kundi hilo ni muhimu nchini Iraq na Syria.

Jenerali Dempsey amesema kuwa kati ya wapiganaji elfu kumi na mbili na elfu kumi na tano kutoka kwa makundi ya upinzani nchini Syria watahitajika katika vita vya nchi kavu nchini Syria.

Idadi hiyo ni mara mbili na hata tatu kwa ukubwa ukilinganisha na idadi inayotarajiwa kupewa mafunzo ya kijeshi mbali na silaha na wanajeshi wa Marekani.