Ebola yatua Marekani

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mgonjwa wa kwanza wa Ebola nchini Marekani

Ugonjwa wa Ebola bado unapasua vichwa vya wanasayansi walio wengi katika kuutafutia chanjo ama tiba ili kukabiliana nao, ingawa mpaka sasa walau kuna matumaini ya dawa ya Zimapp.

Mgonjwa wa kwanza ametambuliwa nchini Marekani eneo la Dallas, Texas mahali amabako utafiti wa kilimo unafanyika .

Mgonjwa huyo aliyegunduliwa bado hajatambuliwa na ametengwa kwa uchunguzi ili kumfuatilia na kuepusha kuambukiza watu wengine.Mtu huyo ametambuliwa jinsi yake kuwa ni mwanamume na alipata uambukizo nchini Liberia na hii ni baada ya kuonesha dalili zote za ugonjwa huo.

Mwanamume huyo anaripotiwa kuondoka nchini Liberia mapema mwezi September na kufika mjini Texas siku iliyofuatia bila ya kuonesha dalili za uambukizo wa virusi hatari vya ugonjwa wa Ebola.Mkurugenzi wa ufuatiliaji magonjwa na udhibiti nchini Marekani Thomas Frieden aliwaambia waandishi habari mapema wiki hii kwamba wote waliotembelea nchini Liberia waligundulika na virusi vya ugonjwa huo nchini Marekani

Mpaka sasa watu zaidi ya 3,000 wamefariki dunia huko Africa Magharibi, na baadhi ya wafanyakazi wa kujitolea kutoka nchini Marekani wamepata ahueni baada ya kurejeshwa nchini Mwao pindi walipogundulika kuwa na dalili za awali za ugonjwa huo.