Omar Gonzalez White House

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mlango huo unavyoonekana

Taarifa kutoka mjini Washngton zinaeleza kua mwanamume mmoja aliyekua ameshikilia kisu mikononi mwake aliruka uzio wa makao ya Rais wa Marekani Brack Obama na kukimbia kuelekea kwenye makazi hayo mwezi huu .

Maafisa wa Ikulu hiyo wamemtambua mtu huyo kua ni Omar Gonzalez,askari wa zamani aliyepigana Iraq, alikua pamoja na kisu,alikuwa akikimbilia katika mlango mkuu wa makazi ya Rais Obama kabla hajakatwa na maofisa wa Ikulu hiyo maarufu kama White House .

Taarifa zinaeleza kuwa kiboksi chenye kengele ya tahadhari kilikuwa kimezimwa .Mkuu wa shughuliza siri za ikulu hiyo Julia Pearson anatarajiwa kuhojiwa kufuatia tukio hilo na jopo la wanasheria.

Wakati hayo yakitukia Rais Obama na familia yake hawakuwa katika Ikulu hiyo.