Facebook yalazimika kuomba radhi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Watu wa jamii hii wanasema wana haki ya kutumia jina ambalo wao hutumia sio lazima liwe lao halisi

Mtandao wa Facebook umewaomba radhi jamii ya wanaume na wanawake waliobadili jinsia yao au (transgender) kwa kusisitiza kuwa lazima watumie majina yao halisi kwenye kurasa sao za mtandao huo.

Kurasa nyingi za watu wa jamii hiyo zilianikwa au kufichuliwa na mtumiaji mmoja mwezi jana kwa kutumia majina bandia.

Akaunti hizo, zilisemekana kuwa bandia kwa sababu wamiliki wake walikuwa wametumia majina yasio yao kama vile, Lil Miss, Hot Mess, badala ya kutumia majina yao halisi kama vile, Bob Smith kwenye kurasa zao.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Facebook imesema itafanyia mabadiliko sera yake ya kujitambulisha kwenye mtandao

Baada ya pingamizi kutoka kwa watu wa jamii hiyo na jamii nzima ya wapenzi wa jinsia moja, Facebook kupitia kwa afisaa mkuu wa mauzo Chris Cox, imetoa taarifa yake na kusema kuwa , itaimarisha sera yake ya ambavyo watu wanastahili kujitambulisha kwenye mtandao wa Facebook katika kurasa au akaunti zao.

''Nataka kuwaomba radhi wale wote waliohisi kutendewa ubaya kutokana na sakata hii.Hii ni kwa sababu Facebook inataka watu watumie majina yao halisi wala sio utambulisho bandia.'' Hata hivyo

Watu hao walikuwa wametishia kuondoka kwenye mtandao huo na kuandaa maandamano makubwa mjini San Francisco.

Msemaji wa watu wa jamii hiyo,Mark Snyder, alisema wameridhika baada ya Facebook kuwaomba radhi.

Alisema kuwa sio watu wa jamii hiyo pekee wanaotaka kutumia majina ambayo sio yao ili kujilinda kutokana na kejeli kwenye mitandao.

Hata hivyo Facebook imekuwa ikisisitiza kuwa watumiaji wa Facebook sharti watumie majina yao halisi ili wapeukane na kejeli kwenye mtandao pamoja na watu kutumia majina yao.