UEFA kuamua mechi ya Man City na CSKA

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mchezaji wa Mancity Yaya Toure

Kilabu ya soka nchini Uingereza Manchester City imesema kuwa itabaini siku ya ijumaa iwapo mechi kati yake na kilabu ya Urusi CSKA Moscow itachezwa katika uwanja usio na mashabiki.

CSKA kwa sasa wanahudumia marufuku ya uwanja wao baada ya visa vitatu vya ubaguzi wa rangi na ghasia kuripotiwa.

Mabingwa hao wa Urusi walicheza mechi yao ya kwanza katika uwanja wa nyumbani katika kundi E dhidi ya Bayern Munich katika uwanja uliokuwa hauna mashabiki.

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA litakutana kuamua iwapo mechi ya Manchester City mjini Moscow ifikiapo tarehe 21 mwezo Octoba itawaruhusu mashabiki au la.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mashamiki wa CSKA Moscow nchini Urusi.

Tukio la ghasia za hivi karibuni zilizoshirikisha Mashabiki wa CSKA lilikuwa katika ufunguzi wa mechi ya kilabu bingwa barani Ulaya mjini Roma mnamo tarehe 17 mwezi Septemba.

Mashabiki wa Urusi walishiriki katika ghasia hizo na polisi ambapo walirusha cheche za moto katika uwanja wa Stadio Olimpiko baada ya kushindwa kwa mabao 5-1.

Ghasia hizo zinajiri baada ya matukio mawili tofauti ya ubaguzi wa rangi katika mechi za kilabu bingwa barani ulaya ikiwemo mechi moja kati ya CSKA na City ambapo Yaya Toure alilalamika kuhusu ubaguzi wa rangi mnamo mwezi Octoba.

Timu hiyo ya Urusi ilipoteza kwa bao moja kwa bila dhidi ya Bayern siku ya jumanne katika mechi ya iliochezwa katika uwanja mtupu.