Joe Biden alazimika kuomba radhi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Joe Biden anasifika kwa kutotafuna maneno yake licha ya hisia zitakazoibuka

Makamu wa Rais wa Marekani, Joe Biden, amelazimika kuwaomba radhi maafisa wakuu wa milki za kiarabu baada ya kusema kuwa utawala huo ndio chanzo cha kuenea kwa itikadi kali za kidini nchini Syria.

Ikulu ya Marekani ilithibitisha kuomba radhi kwa UAE siku ambayo pia Biden alilamika kuomba Uturuki radhi kwa matamshi ya kukera.

Maafisa wakuu katika Milki za Kirabau walilaani matamshi ya Biden aliyotoa kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Harvard wiki jana.

Milki za kirabu ni moja ya mataifa ya kiarabu yaliyoungana na jitihada za Marekani dhidi ya wapiganaji wa IS nchini Syria na Iraq.

Wanajeshi wa mataifa hayo wamekuwa wakishambulia wapiganaji wa kiisilamu IS ambao wanadhibiti sehemu kubwa ya Iraq na Syria katika wiki chache zilizopita.

Bwana Biden aliambia wanafunzi wa Harvard siku ya Alhamisi kuwa Uturuki , Milki za kirabau na Saudi Arabia zimetoa mabilioni ya dola za kununua zana za kivita kwa wapaiganaji wa Sunni wanaopambana na wanajeshi wa Rais wa Syria Bashar al-Assad.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (kulia) alisemekana kukasirishwa na matamshi ya Joe Biden

Alimpigia simu mwanamfalme wa Saudi Abu Dhabi, Mohamed bin Zayed Al Nahyan, mnamo siku ya Jumapili kumuomba radhi baada ya utawala katika Milki za kirabu kumtaka kufafanua alichokisema bwana Biden.

Matamshi ya Biden yalikuwa: ''ya kustaajabisha na yaliyolenga kupuuza mchango wa Milki za kiarabu katika vita dhidi ya makundi yanayoeneza itikadi kali za kidini na ugaidi nchini Syria, ''lilinukuu shirika kitaifa la habari la WAM.

Ni mara ya pili katika siku mbili kwa bwana Biden kutakiwa kufafanua matamshi yake kwa mataifa mawili kuhusiana na vita vya IS.

Mnamo siku ya Jumampsi, alimpigia simu waziriu mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, baada ya kughadhabishwa na matamshi ya Biden akisema ikiwa Biden anaweza kutumia matamshi kama hayo basi hamthamini hata kidogo.

Ni kaiwaida kwa Biden kuwa mwazi na kutotafuna maneno yake.