Wafanyakazi warejea kazini Hong Kong

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Hong Kong

Wafanyakazi wa umma katika eneo la Hong Kong wamerejea kazini pamoja na kuendelea kwa maandamano yaliyodumu kwa zaidi ya wiki moja kisiwani humo na kulifanya eneo shughuli za uzalishaji kuathirika.

Hata hivyo idadi ya waandamanaji katika mitaa ya eneo hilo imepungua kwa mamia ikilinganishwa na siku za awali maandamano hayo yalipoanza.

Serikali nchini humo imewataka raia hao kusitisha maandamano ifikapo leo siku ya jumatatu na kwamba wasipofanya hivyo hatua kali za kuzima maandamano zitachukuliwa japo kuwa hakuna dalili kama polisi wanajiandaa kuingia eneo la waandamanaji.Waandamanaji hao wanapinga hatua ya serikali ya China kuwachagulia kiongozi wao katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika 2017.