IS wakaribia kuteka mji muhimu Syria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mji wa Kobane unakabiliwa na hatari ya kutekwa na wapiganaji wa Islamic State

Afisa mmoja katika mji wa wakurdi wa Kobane uliopo ndani ya Syria , karibu na mpaka wa Uturuki amebainisha kuwa unakabiliwa na hatari kubwa ya kutekwa na wapiganaji wa Islamic State baada ya makabiliano yaliyodumu kwa wiki tatu sasa.

Bendera ya Islamic State imekuwa ikipeperushwa kwenye jengo moja la mji lililoko mashariki mwa nji huo.

Afisa huyo Idriss Nassan ameiambia BBC kuwa vikosi vya Islamist vimechukua udhibiti wa eneo muhimu la mlima Mistenur ulioko juu ya mji wa Kobane na kuongeza kuwa makombora ya Islamic State sasa yanafikia maeno yote ya mji .

Sauti ya Milio ya makombora sasa inasiskika na moshi mkubwa wa makombora hayo umetanda kwenye anga ya mji huo wa Kobane hali inayoonyesha kuwa hali inaendelea kuwa mbaya.

Mkuu wa zamani wa majeshi nchini Uingereza , Generali Lord Richards, ameelezea hofu yake kuwa mashambulizi ya anga dhidi ya Syria na Iraq hayatatosha kuwashinda Islamic State.

Generali Richards, ambaye alikuwa mkuu wa majeshi kati ya mwaka 2010 na 2013, amesema maelfu ya wanajeshi wa magharibi watahitaji kupata mafunzo na usaidizi kwa majeshi ya ndani ya nchi hizo ili kuwashinda Islamic state.

Aidha General Richards, amesema anahofu kuwa baadhi ya viongozi wa dunia hawafahamu vyema hatari inayoweza kutokea kwa kutumia mashambulio ya anga dhidi ya ICC