Mpishi amchinja na 'kumpika' mpenziwe

Image caption Volke alimchinja na kumkatakata mpeni wake na kisha kupika sehemu za mwili wake

Mwanamume ambaye kazi yake ni ya upishi nchini Australia, anadaiwa kumuua mpenzi wake na kumkatakata vipande na kupika baadhi ya sehemu zake za mwili.

Aliyafanya unyama huo kabla ya yeye mwenyewe kujitoa uhai wake.

Marcus Volke, mwenye umri wa miaka 28, alijikataa koo yake huku akiwatoroka polisi waliokuwa wamekuja kufanya uchunguzi baada ya majirani zake kuripoti kuwepo harufu mbaya mfano wa nyama iliyooza iliyokuwa inatoka nyumbani kwa mwanamume huyo.

Maafisa wa polisi walipata sehemu za mwili wa mwanamke huyo zikitokota kwenye sufuria iliyokuwa imejazwa kemikali huku vipande vingine vikiwa kwenye karatasi za plastiki za takataka nje ya nyumba katika mtaa wa kifahari za Teneriffe.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa jarida la Brisbane Courier Mail. Mwanamke huyo raia wa Indonesia bado hatajambulishwa rasmi.

Wapenzi hao waliokuwa wanaishi pamoja walikutana wakiwa wanafanya kazi kwa meli za kifahari na wote walikuwa wameajiriwa.

Wakazi wa mtaa huo waliambia vyombo vya habari kuwa harufu mbaya ilikuwa inatoka katika myumba ya Volke na ikazidi kuwa mbaya siku ziliposonga.

"nilipotoka nje harufu hiyo ilisababisha machozi kutoka machoni na hata kunifanya kujihisi mgonjwa,'' alisema mkazi mmoja. ''Ungedhani chakula cha Mbwa au nyama ilikuwa imeachwa nje kwa siku kadhaa.''

Polisi wangali wanafanya uchunguzi.