Canada kukabiliana na IS

Haki miliki ya picha AFP
Image caption IS

Nchi ya Canada imekuwa nchi ya hivi karibuni kuungana na majeshi yanayokabiliana na wapiganaji wa Islamic State IS nchini Iraq.

Bunge la Canada limepiga kura kupitisha uamuzi wa kutoa hadi ndege sita za kivita na wanajeshi 600 kukabiliana na wapiganaji hao. Agenda hiyo ya Canada kuunga mkono majeshi ya Marekani na Uingereza kupeleka vikosi kukabilaiana na wapiganaji wa IS kwa muda mrefu imekuwa ikipingwa na wabunge wa upinzani nchini humo lakini kwa sasa wamepitisha uamuzi huo.

Uamuzi huo wa Canada unakuja siku moja chache baada ahadi kama hiyo kutoka nchini Australia kuungana na wanajeshi kutoka nchi mbalimbali za ulaya.