Kobane yatakiwa kulindwa dhidi IS

Haki miliki ya picha AFP GETTY
Image caption kabone

Mjumbe wa umoja wa mataifa nchini Syria Staffan de Mistura amesema kuwa dunia inapaswa kufanya kila linalowezekana kuwazuia wapiganaji wa kundi la Islamic state IS wanaotaka kuuchukua mji wa Kobane.

Staffan amiambia BBC kuwa iwapo mji wa Kabone utatekwa na wapiganaji hao maafa makubwa yatatokea na kuleta madhara pia katika eneo jirani la Uturuki.

Amesema kuwa hatua zinapaswa kuchukuliwa kudhibiti hali hiyo.Kamanda wa Wakrud katika eneo la Kabone amesema mashambulizi ya anga yaliyofanywa na dhidi ya wapiganaji hao.

Hata hivyo ameelezea umhimu wa kuimarisha vikosi vya ardhini ili kuwakabili wapiganaji wa Islamic State.