Hong K:Wanafunzi kuandamana tena

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption waandamanaji Hong Kong

Serikali ya eneo la Hong Kong imeitisha mazungumzo maalumu na viongozi wa wanafunzi ambao wamekuwa wakiratibu maandamano yaliyodumu kwa wiki mbili hadi sasa.

Mkutano huo wa serikali ya eneo hilo na wanafunzi unatarajiwa kufanyika leo.waandamanaji hao wanapinga utawala wa Beijing kuwachagulia mgombea katika uchaguzi mkuu wa eneo hilo 2017.

Hata hivyo wanafunzi hao wamesisitiza kuwa wataendelea na mgomo huo pamoja na serikali hiyo kuhitaji mazungumzo na viongozi wao.

Waandamanaji hao kwa sasa wamekuwa wakiendelea na maandamano huku baadhi ya huduma mhimu na kazi zikidorola.