Mkono bandia ulio na hisia wavumbuliwa

Haki miliki ya picha LEFEHAND2
Image caption Mkono bandia

Uvumbuzi wa mkono bandia umerejesha hisia za wagonjwa wawili kuweza kugusa baada ya mwaka mmoja, kulingana na ripoti ya wanasayansi wa Marekani.

Wawili hao sasa wanaweza kutunda matunda bila tatizo lolote.

Kwa mujibu wa jarida la tiba ya sayansi, sensa zilizopo katika mkono huo bandia hutumiwa kutuma ishara moja kwa moja katika mwili.

Haki miliki ya picha LIFEHAND
Image caption Mkono bandia

Wakati huohuo kundi moja la wanasayansi wa Sweden limefanya uvumbuzi mwengine wa viungo bandia,unaoshikanisha mkono huo bandia moja kwa moja na mfupa ili kuimarisha udhibiti.

Mmoja wa watu waliofaidika na uvumbuzi huo wa Marekani ni Igor Spetic aliyepoteza mkono wake wa kulia kupitia ajali miaka minne iliopita.

Aliwekewa mkono wa bandia lakini hakuweza kuhisi chochote.

Haki miliki ya picha
Image caption Mkono bandia

Ilimbidi awe mwangalifu katika chochote kile alichokuwa akifanya na kuweza kutumia macho yake kubaini iwapo alikuwa akitumia nguvu au la wakati anaposhika kitu.

Lakini kundi moja la wanasayansi katika chuo kiikuu cha Case Western Reserve liliweka sensa katika mkono huo wa bionic ambayo iliweza kutuma ujumbe wa msisimuko wa kielektroniki katika ubongo wake.

Itikio la ubonge liliweza kutuma ujumbe katika maeneo 19 ya mkono kutoka katika kiganja hadi katika dole gumba.

Hatua hiyo ilimwezesha bwana Spetic kujua iwapo anashikilia kitu au la.Mtu huyo ameweza kuutumia mkono huo kwa miaka miwili na nusu.