Somalia yafunga balozi 9

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Baadhi ya balozin zimekuwa zikisimamiwa na mabalozi bandia waliojibandika tu vyeo

Balozi 9 za nchi ya Somalia zimefungwa katika mataifa kadhaa ya ng'ambo.

Waziri wa mambo ya nje wa Somalia Abdirahman Duale Beyle amesema serikali haiwezi tena kumudu gharama za uendeshaji wa balozi hizo.

Wadadisi wanasema baadhi ya balozi hizo zimekuwa zikiwekwa wazi na watu waliojibandika vyeo vya mabalozi wakati Somalia haikuwa na serikali kwa zaidi ya miaka 20 tangu kuanguka kwa utawala wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Siad Barre hapo 1991.

Serikali ya sasa ambayo imeanza kufanya kazi miaka miwili iliyopita ndiyo inayotambuliwa na mataifa makubwa kama vile Marekani na aUingereza.