Tumbaku chanzo cha maradhi ya zinaa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Virusi vyanavyoambukizwa kwa njia ya zinaa vya HPV16 vilipatikana kwa wavutaji sugu wa sigara

Sigara na bidhaa nyinginezo za Tumbaku, zinasemekana kuongeza uwezekano wa mtumiaji kuambukizwa virusi vinavyooambukizwa kwa njia ya zinaa vinavyohusishwa na Saratani ya Koo na Mdomo .

Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na wanasayansi nchini Marekani.

Virusi hivyo vijulikanavyo kama 'Oral human papilloma virus aina ya 16 au HPV16, vinapatikana katika asilimia 80 ya watu wanaougua Saratani ya koo na vinaambukizwa kwa ngono nzembe.

Visa vya Uvimbe wenye Saratani na ambao unasababishwa na virusi hivyo, vimeongezeka kwa asimilia 225 nchini Marekani katika miongo miwili iliyopita.

Watafiti waligundua kuwa virusi vya HPV16 vinapatikana sana kwa watu wanaovuta sigara au wanaotumia bidhaa nyinginezo za Tumbaku ingawa pia watu wasiovuta sigara wako katika hatari ya kuambukizwa virusi hivyo.

Watafiti hao wanasema utumiaji wa sigara unawaweka watumiaji katika hatari ya kuambikizwa virusi hivyo vya HPV16 na ingawa haijulikani sababu , wansayansi hao wanashuku kuwa virusi hivyo huwa sugu kwa wavutaji sigara.

Utafiti huo ulifanyiwa watu 6,887 nchini Marekani.

Miongoni mwa watu hao, 2,012, walikuwa wavutaji wa sigara na pia walitumia bidhaa nyingezo za Tumbaku.

Watafiti waligundua virusi hivyo kwa kuchunguza damu na mkojo wa wavutaji sigara na miongoni mwa wavutaji wa sigara vilipatikana kwa wingi hasa kwa wale waliovuta sigara zaidi ya mara nne kwa siku.

Kwa watu hawa tisho la kupatikana na virusi vya HPV16 ilikuwa wazi sana kwa asilimia 31. Kwa wavutaji sugu, tisho la wao kupatikana na virusi hivyo ilikuwa asilimia 68.

Virusi vya Human Papiloma vinaweza kusababisha Saratani ya kizazi kwa wanawake.