Suluhu mgogoro Hong Kong mashakani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waandamanaji Hong Kong

Waandamanaji wanaopigania demokrasia katika eneo la utawala la Hong Kong nchini China "wamesikitishwa" japo hawajashangazwa na hatua ya serikali ya utawala wa eneo la Hong Kong kufuta mazungumzo na wanafunzi hao ili kutatua mgogoro uliotikisa eneo hilo kwa karibu wiki mbili. Amedai mwanafunzi mmoja.

Mwanafunzi mwandamanaji Harold Li ameishtumu serikali kwa kushindwa kuupatia ufumbuzi mgogoro huo, ambao umeshuhudia maelefu ya watu wakiingia mitaani kuandamana.

Hong Kong imewalaumu wawakilishi wa wanafunzi kwa "kupuuza" msingi wa kuwepo kwa mazungumzo yenye tija kati ya pande mbili hizo.