USA:Kuwakagua raia wa mataifa ya ebola

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ukaguzi wa ebola katika uwanja wa ndege

Mpango mpya wa ukaguzi umetangazwa nchini Marekani kujaribu kupunguza kuwasili kwa wageni walio na ugonjwa wa Ebola.

Wasafari ambao wanawasili mjini New York kutoka nchi tatu zilizoathiriwa zaidi na ugonjwa wa Ebola Magharibi mwa Afrika kama vile Guinea, Liberia na Sierra Leone watafanyiwa ukaguzi

Programu hiyo pia inatarajiwa kupelekwa kwenye viwanja vyengine majuma yajayo.

Nchini Uhispania takriban watu 17 wametengwa baada ya wao kukaribiana na muuguzi ambaye sasa ni mgonjwa sana hospitalini.

Morocco nayo inasema kuwa inataka kuahirisha mashindano ya kuwania klabu bingwa barani Afrika kutokana na hofu ya ugonjwa wa Ebola.