IS yashambulia kivuko cha Uturuki

Haki miliki ya picha AP
Image caption Islamic state

Afisa wa ngazi ya juu kwenye mji wa mpaka wa Kobane nchini Syria amiambia BBC kuwa wanamgambo wa Islamic State wamejaribu kukishambulia kivuko cha mpaka na Uturuki lakini wakashindwa kukidhibiti kivuko hicho.

Khalid Berkel amesema kuwa wanamgambo hao wameshambulia mji wa kobane kutoka pande tofauti katika jitihada za kuuzingira kabisa ambapo wamepiga hatua kutoka maeneo ya mashariki kwa kutumia mabomu yaliyotolewa kwenye magari.

Wapigani wa kikurdi na wanajeshi huru nchini Syria wanasema kuwa wanahitaji kwa dharura silaha nzito.

Maelfu ya raia wamekwama kwenye miji wa kobane na umoja wa mataifa umeonya kuwa kutatokea mauaji ya halaiki iwapo mji huo utatekwa .

Awali wito ulitolewa nchini Syria na Iraq wa hatua za dharura kuchukuliwa dhidi ya wanamgambo hao

Vyombo vya habari vinasema kuwa maafisa nchini Iraq kwenye mji ulio magharibi mwa Anbar wameitaka serikali yao kuomba msaada wa vikosi vya nchi kavu vya Marekani katika vita dhid ya ISIS.