Chanjo yapata ukinzani Kenya

Image caption Viongozi wa kanisa wanasema chanjo hiyo ni njama ya kuwapa sindano za mpango wa uzazi wanawake

Nchini Kenya kumekuwa na mvutano kati ya Kanisa Katoliki na wizara ya afya kuhusu uhalali wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa pepopunda.

Serikali ya Kenya inanuia kutimza lengo la kuangamiza ugonjwa huo miongoni mwa raia , hata hivyo Kanisa Katoliki limepinga vikali hatua hiyo likisema chanjo hiyo ina madhara kwa afya ya uzazi kwa wanawake.

ukiwa ni mpango wa serikali ya Kenya kuboresha afya ya uzazi,kwa akinamama walio chini ya miaka 19 hadi 49 watapokea chanjo kuzuia pepopunda hata hivyo si wote wanaitazama chanjo hii kwamba ina lengo la kuokoa maisha ya mama.

Kanisa Katoliki nchini Kenya limewataka waumini wake kuisusia chanjo hiyo , na huenda ikawa sababu kubwa ni pale ambapo shirika la Afya WHO lilikua katika harakati za kutengeneza chanjo ya kuzuia kupata mimba.Na mnamo mwaka 1993 shirika hilo liliidhinisha mataumizi ya chanjo ya pepo punda.