Kim Jong-un:Anaugua au kang'olewa?

Haki miliki ya picha afp getty
Image caption Kim Jong Un sasa amekosa hafla mbili muhimu za kiserikali katika ratiba ya kitaifa

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, ametoweka hadharani kwa takriban siku 38 na kuzusha tetesi nyingi kuhusu hali ya utawala katika nchi inaosifika sana kwa usiri wake.

Hasahasa kutohudhuia kwake katika hafla mbili kuu za kuadhimisha siku ya kuundwa kwa chama tawala cha "Wafanyakazi"na ile ya kuasisiwa kwa taifa la Korea Kaskazini ambapo kaawaida kiogozi huyo angetazamiwa kuhudhuria.

Hii imetafsiriwa na baahi ya watu kua ni ishara ya kuwepo mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali vinadai kutoonekana kwake hadharani ni kutokana na sababu za kibinafsi.

Image caption Bwana Kim alirithi mamlaka kutoka kwa babake Kim Jong-il

Wachambuzi wa kigeni wanadadisi sababu hizo kua ni za kiafya kuanzia matatizo ya kisukari,uvutaji mwingi wa sigara na hata maumivu aliyoyapata hivi karibuni alipoteguka kifundo cha mguu wakati anakagua gwaride la kijeshi.

Hata hivyo baadhi ya wadadisi wanasema Kim kwenye umri wa miaka 32 huenda anakabiliwa na njama za mapinduzi na hata inawezekana yuko katika kizuizi cha nyumbani baada ya kuondolewa madarakani na vigogo wa chama na jeshi.

Inaarifiwa wameshtushwa na tabia yake ya kuwafyeka wapinzani wake wa kisiasa hasa kuuwawa kwa mjomba wake Jang Song-taek Desemba 2013 - na kushindwa kwake kuchepua ufanisi wa kudumu kwa uchumi wa nchi hiyo.

Hata hvyo licha ya tetesi za kuwepo njama za mapinduzi,makachero wa Korea ya Kusini wanaamini kwamba Kim anauguza maradhi na kwambna uamuzi wa kupunguza shughuli zake hadharani huenda kukatokana na juhudi za kutaka kudumisha ile dhana kwamba enzi ya ukoo wa Kim haiwezi kukosekana katika Korea Kusini.

Image caption Kim Jong-un ana umri wa miaka 32 na kuna tetesi kuwa dadake mdogo amechukua madaraka

Kumekuwepo na tetesi kwamba dadaake mdogo Kim, Kim Yo-jong, huenda anashikilia kwa muda madaraka ya kaka yake,lakini hata kama ni kweli haiyumkini atakubalika katika jamii ambayo hadhi ya mwanamke bado ni duni na haioni sababu ya kuongozwa na mwanammke.

Kwa hivyo pindi akirejea hadharani ,kinachotarajiwa ni harakati zaidi za kidiplomasia zikiambatana na vitisho na mbwembwe za kijeshi na kisiasa kuonyesha kuwa taifa la Korea ya Kaskazini bado ni taifa lenye nguvu ambalo haliwezi kudharauliwa wala kupuuzwa.