Obiang arejesha mali za E. Guinea

Image caption Teodorin Obiang mtoto wa rais wa Equatorial Guinea

Mtoto wa rais wa Equatorial Guinea amekubali kutoa mali yenye thamani ya zaidi ya dola milioni thelathini zilizoko nchini Marekani ambazo serikali ya Equatorial Guinea inasema zilinunuliwa kutokana na fedha iliyoporwa kutoka vyanzo vya fedha vya nchi hiyo.

Tay-a-DOOR-oh, un-GAY-mu, Obiang, Mahn-gay amekubali kuuza kasri yake ya Malibu na vitu binafsi ikiwemo vya kumbukumbu ya mwanamuziki mashuhuri duniani, hayati Michael Jackson, na kwenda nchini Equatorial Guinea kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji nchini humo.

Teodorin Obiang ni makamu wa pili wa rais wa Equatorial Guinea, na mtoto wa kiume wa rais, ambaye amekuwa akifuatiliwa na serikali ya Marekani na Ufaransa kutokana na manunuzi yake ya kifahari ambayo yanadaiwa malipo yake yalitokana na fedha iliyoibwa serikalini.

Kama sehemu ya kuipatia ufumbuzi kesi hii, iliyofunguliwa katika mahakama ya California, jumba lake la Malibu linaloangaliana na bahari likiwa na thamani ya dola milioni thelathini litauzwa kama ilivyo kwa glovu iliyokuwa ikivaliwa na Michael Jackson, ikiwa imenunuliwa katika mnada kwa mamilioni ya dola.

Teodorin Obiang amekubali kulipa dola milioni 20 kwa shirika na hisani, ambalo litatumia fedha hizo kuwanufaisha wananchi wa Equatorial Guinea.

Zaidi ya dola milioni kumi zitachukuliwa na serikali ya Marekani, ambayo wizara ya Sheria imesema zitatumika kuinufaisha nchi hiyo ya bara la Afrika kwa ruhusa ya sheria na fedha nyingine zitatumika katika shughuli za hisani. Bwana Obiang amesema anafurahi kuona mwenendo wa kesi hiyo umemalizika, lakini amesema fedha hizo zimepatikana kutokana na sheria za nchi hiyo.