Mabinti wa Chibok bado wanashikiliwa

Haki miliki ya picha afp
Image caption Aliyekua kiongozi wa Boko Haram, Aboubakr Shekahu

Walikamatwa na kikundi cha kigaidi cha kiislam boko Haram kutoka shuleni kwao huko chibok.

Ingawa kunaahadi nyingi kutoka serikali ya Nigeria kwamba wataokolewa na pia watapewa msaada kutoka dunia nzima lakini mpaka sasa bado hawajaonekana, ripoti ya mwandishi wa BBC Will Ross kutoka Lagos inasomwa na Regina Mziwanda

Miezi sita sasa na wasichana 219 bado wametekwa, ni ushaidi mdogo sana unaojulikana kwa kile kilichotokea kuhusu wao tangu walipotekwa wakiwa katika shule yao ya bweni huko Chibok na Boko Haram.

Serikali ya Nigeria imepata wakati mgumu sio tu kuwaokoa lakini pia kwa kuonyesha mwitikio mdogo wa umma

Wazazi wa Chibok wameiambia BBC kuwa wameachwa na maneno tu na ahadi zinazovunjwa kwamba watoto wao wa kike watarudi nyumbani hivi karibuni, baba mmoja amesema wanasiasa wamejikita kwenywe uchaguzi wa mwakani ujao zaidi yakuwaokoa watoto wao waliopotea.

Tangu mwezi April vijana wengi wa kike na wa kiume wametekwa nyara na kikundi cha kiislam cha Boko haram ambao wanaongoza mijini na vijijini karibu na mpaka wa Cameroon.

Serikali ya Nigeria imesema jeshi kwa sasa limepata mafanikio dhidi ya vita na boko haram lakini wamezidiwa nguvu kaskazini mashariki ambapo raia hawako salama na maelfu ya watu wamehama makazi yao katika wiki za hivi karibuni.