Ajikuta na mdudu mnyonyaji puani

Haki miliki ya picha CATERS
Image caption Mwanadada Daniela aliishi na mdudu huyo kwenye pua lake kwa mwezi mmoja

Mwanamke mmoja aliyekuwa amesafiri kwenda Kusini mwa Bara Asia, alishtuka alipogundua kuwa mdudu anayeitwa Kaka au 'Leech' kwa kimombo na ambaye hunyonya damu alikuwa anaishi katika pua lake.

Mdudu huyo alikuwa na urefu wa nchi 3. Mwanadada huyo aligundua uwepo wa mdudu huyo katika pua lake baada ya kurejea kutoka katika safari yake ya bara Asia.

Daniela Liverani, mwenye umri wa miaka 24, kutoka mjini Edinburgh, Scotland, amekuwa akivuja damu kutoka katika pua lake kwa wiki kadhaa.

Hata hivyo alidhani labda mshipa mdogo wa pua lake ulikuwa umepasuka baada ya kupata ajali akiwa anaendesha pikipiki.

Bi Liverani alikuwa bafuni wiki jana Alhamisi alipogunduya mdudu huyo kwenye pua lake alipoona kitu kikionekana kikisonga songa katika pua lake.

Wahudumu wa hospitali, walitumia vifaa vidogo kumuondoa mdudu huyo kutoka katika pua la Daniela.

Bi Liverani anaamini kuwa mdudu huyo aliingia katika pua lake alipokuwa safarini Vietnam au Cambodia lakini hata alipohisi kitu kikitembea kwenye pua lake alidhani labda ilikuwa damu iliyokuwa imeganda.

''Mimi nilidhani tu ilikuwa damu iliyokuwa imeganda,kwenye pua langu,'' alisema Daniela.

Wakati Bi Liverani alipoingia bafuni ndipo mdudu huyo alioenakana kwa haraka kwa sababu ya mvuke uliotokana na maji moto ambayo yaliwezesha mdudu huyo kuteleza.

Hata hivyo alipogundua mdudu huyo alikwenda hadi hospitalini ambako mdudu huyo alitolewa kwenye pua la mwanadada huyo.

''Madaktari walifanya kazi nzuri sana, ninawapongeza, kwa sababu sio kawaida kwao kuona kitu kama hiki kila siku,'' alisema Liverani.