Uholanzi hoi Kombe la Ulaya

Image caption Timu ya Uholanzi

Kitimtim cha kutafuta tiketi ya kuelekea nchini Ufaransa kwaajili ya michuano ya soka barani Ulaya mwaka 2016 iliendelea tena usiku wa kuamkia leo huku nyasi za viwanja kadhaa zikiwa katika wakati mgumu.

Katika kitimtim hicho timu ya Uholanzi iliwanyima raha mashabiki wake baada ya kukubali kupokea kipigo cha mabao 2-0, kutoka kwa Iceland. Nayo Wales ikautumia vema uwanja wake wa nyumbani baada ya kuigalagaza Cyprus kwa jumla ya mabao 2-1.

Italy ilikuwa ugenini dhidi ya Malta huku mchezo huo ukimalizika kwa kila timu kucheza pungufu baada ya wachezaji wao kuoneshwa kadi nyekundu.

Michael Misfud wa Malta alikuwa wa kwanza kwenda nje katika dakika ya 27 huku Leonardo Bonucci wa Italy akifuatia katika dakika ya 73 ya mchezo, hadi mwisho wa kipute hicho Italy ikawabanjua wapinzani wao bao 1-0.