Ebola na Vibweka vyake

Mnyoo wa Ebola

Chanzo cha picha, Thinkstock

Maelezo ya picha,

Mnyoo wa Ebola

Mwanafunzi wa shahada ya pili kutoka nchini Sierra Leone amedai kwamba amekua akikataliwa kuishi katika maeneo mengi katika jiji la Norwich kwa kumhofia kuwa huenda ana virusi vya ugonjwa wa Ebola .

Mwanafunzi huyo ambaye pia nim mtangazaji wa redio na ameshawahi kufanya kazi na BBC Media Action anadai kuwa kukataliwa huko kuna kumemfikia kwa njia ya barua inayoeleza kwamba wa Norwichhawatampokea mtu yeyete anayetokea ama kuishi mpakani na nchi zilizokumbwa na ugonjwa wa Ebola ama atakaye zitembelea nchi za Africa Magharibi siku zijazo.

Kuanza masomo katika chuo kikuu ni wakati mzuri wa furaha na matarajio makubwa baada ya chuo na maisha bora lakini kwa Amara Bangura imekua ni tofauti kabisa.

Yeye amekua akikataliwa kuishi kila mahali kwasababu ni raia wa mojawapo ya nchi zilizokumbwa na ugonjwa huo , Sierra Leone.

Amara aliwasili mjini Norwich akitokea Africa Magharibi siku arobaini zilizopita na akumbana na kikwazo cha kukataliwa na wenye nyumba za kupangisha na mmoja akamkataa kwa barua

Barua hiyo ilisomeka hivi, katika mazingira yasiyokuwa ya kawaida,maelezo yako yanaonesha unastahili kuwa mpangaji wetu ,

Hata hivyo,ulimwengu unatambua kinachoendelea na matokeo ya ugonjwa wa Ebola,tumeamua kutokukupokea sio wewe tu bali hata wengine wanaotokea ama karibu na Africa Magharibi katika kipindi cha miezi miwili iliyopita ama hata kutembelea maeneo hayo wakati ujao.

Ingawa walimpa sharti la kuwapa pasi yake ya kusafiria ndipo wampangishe lakini walipogundua anatokea Africa Magharibi mahali ambako ugonjwa umetua siku za hivi karibuni walimkataa.

Si sawa ,na kama utafikiri kwamba kila mtu anayetoka Sierra Leon ameathirika,sio sawa kabisaaa,na kukataliwa huko kumemchanganya anasmea Amara Bangura.

Amara ana umri wa miaka 35,amesema ni kosa kufikiria tu kuwa watu kutoka Sierra Leone wana ugonjwa huo.

Lakini habari njema kwa upande mwingine wa Amara ni kwamba baada ya kutafuta makaazi kwa wiki kadhaa,amepata mahali pa kuishi na hivyo ataendelea na masomo yake.

Mpaka sasa zaidi ya watu elfu nne na mia nne wamesha fariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola kwa kiasi kikubwa ni kutoka Africa Magharibi.

Nchi ya uingereza imechukua tahadhari juu ya ugonjwa huo na hivyo imeanza kuwachunguza abiria wanaoshukia katika uwanja wa ndege wa

Heathrow ikiwa wameambukizwa ama dalili za ugonjwa wa Ebola.

Na wale wote wanaotoka katika nchi zilizoathiriwa na ugonjwa huo watahojiwa na kupimwa joto miilini.