Waendesha mashitaka:Pistorius aende jela

Image caption Oscar Pistorius akitoka mahakamani,Pretoria, Afrika Kusini

Waendesha mashitaka wamekuwa wakipanga hoja zao dhidi ya mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius ili aweze kutumikia kifungo jela kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Shahidi wa kwanza upande wa mashitaka katika kikao cha kusikiliza hukumu alikuwa Kim Martin, binamu yake Bi Steenkamp.

Pistorius alipatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia Bi Steenkamp mwezi uliopita - lakini aliondolewa mashitaka ya kuua kwa kukusudia.

Wakati huo huo familia ya Steenkamp imetoa taarifa mpya ikisema hawahitaji pesa kutoka kwa Pistorius.

Kikao cha kusikiliza hukumu kimeahirishwa Jumatano na kinatarajiwa kuendelea Alhamisi.