Kiongozi wa MRC mahakamani Kenya

Image caption Kiongozi wa MRC Omar Mwamnuadzi

Kiongozi wa kundi linalotaka kujitnga kwa jimbo la Pwani nchini Kenya, ameshtakiwa kwa kosa la kuanda a mkutano wa hadhara bila kibali na pia kwa kutatiza amani.

Omar Mwamnuadzi alikanusha madai hayo alipofikishwa mahakamani Jumatano jioni.

Alikamatwa pamoja na watu wengine 11 wa vuguvugu lao la Mombasa Republican Council (MRC) kufuatia msako wa polisi.

Serikali iliharamisha kundi la MRC na kulitaja kuwa la kigaidi kufuatia harakati zao za kutaka eneo la Pwani kujitenga na Kenya.

Hata hivyo mahakama ilibatilisha uharamu wa kundi hilo mwaka 2012.

MRC likanausha madai ya serikali kuwa limekuwa likishirikiana na wapiganaji wa al-Shabab kufanya mashambulizi Kenya.

Kadhalika kundi hilo limekuwa likilaumu serikali kwa kutenga watu wa pwani ya Kenya ambako watu wengi ni waisilamu na kuwapa ardhi watu wa kutoka nje ya jimbo hilo au wageni.

Pwani ya Kenya ndio kitovu cha utalii nchini Kenya.

Inaarifiwa kiongozi huyo pamoja na wenzake walipatikana na nyaraka zilizoandikwa kwa lugha ya kiarabu na polisi wametaka nyaraka hizo kutafsiriwa.