Ebola yasitisha caf 2015

Haki miliki ya picha CAF
Image caption CAF

Kasi kubwa ya usaambaji wa virusi vya ugonjwa wa Ebola imesababisha michuano ya kombe la mataifa ya Africa mashakani na hivyo kuahirishwa mpaka mwakani.

michuano hiyo ilipaswa kupigwa katika nchi ya Morocco mnamo tarehe kumi na saba ya mwezi wa kwanza,na serikali ya Morocco iliwaambia waandaaji ya kwamba inataka kuahirisha michuano hiyo sababau ya kasi ya ugonjwa huo.

Serikali hiyo imezingatia hatari iliyowekwa wazi na mashabiki kutoka katika nchi za Africa Magharibi.nayo bodi ya utendaji inayoongozwa na shirikisho la soka barani Africa CAF inatarajiwa kufanya maamuzi yake ya mwisho mwezi ujao,

ingawa mpaka sasa shirikisho hilo limebaki na msimamo wake kwamba michuano hiyo iendelee kama kawaida.