Polisi Brazil yamkamata muuaji

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Tiago mikononi mwa polisi

Polisi nchini Brazili wamemkamata mwanamume mmoja aliyekiri kwa kinywa chake kuua watu wapatao thelathini na tisa katika kipindi cha miaka mitatu.

Polisi wamemuelezea mtu huyo kuwa ni mwenye umri wa miaka ishirini na sita ambaye alikua mlinzi katika kampuni fulani alikuwa akiwawinda wa watoto wa mitaani,wanawake na wapenzi wa jinsia moja.

Mwanamume Tiago Gomes da Rocha alikamatiwa nyumbani kwake Goiania na polisi wa kikosi maalumu waliokuwa wakichunguza mauaji hayo,na kuelezea namna walivyomtia mkononi kuwa alihemewa na aliyoyafanya,

Kijana huyo alikuwa akitekeleza mauaji yake kwa kutumia pikipiki huku akiwa ameuficha uso wake kwa kutumia kofia ngumu ya pikipiki na kuwashambulia alowalenga, na akikutana nao huwadai walichonacho kabla hajawapiga risasi na kuwaacha wakijifia taratibu.