kamati mpya ya Ebola yateuliwa S.Leone

Haki miliki ya picha
Image caption Waasi

Ripoti kutoka Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo zinasema kuwa watu wanaokisiwa kuwa wanachama wa kundi la waasi kutoka nchini Uganda wamefanya mashambulizi mengine katika eneo lililo mashariki mwa nchi ambapo wamewaua takriban watu 20

Shirika moja la kutetea haki za kibinadamu linasema kuwa waasi kutoka kundi la Allied Democratic Forces ADF ndio walihusika na shambulizi hilo kwenye kijiji kilichopo katika mkoa wa kivu Kaskazini.

Siku ya Alhamisi watu 26 waliuawa kwenye mji ulio mashariki mwa DRC wa Beni karibu na mpaka na Uganda.

Wengi waliouwa ni raia wakiwemo watoto.