Hong Kong:Serikali kufanya mazungumzo

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Katibu wa eneo la Hong Kong

Mkurugenzi mkuu wa mji wa Hong Kong Carrie Lam ametangaza kuwa serikali itafanya mazungumzo na viongozi wa wanafunzi siku ya jumanne.

Wanakarati wanaopigania demokrasia mjini Hong Kong wamedhibiti tena maeneo yao huku kukiripotiwa makabiliano na polisi .

Maelfu ya waandamanaji wengine waliokuwa wamevaa miwani ya kujikinga walijenga upya vizuizi katika wilaya ya Mong Kok.

Polisi walijibu kwa kutumia marungu na maji ya kuwasha. Maafisa 15 wameripotiwa kujeruhiwa huku wengine 26 wakikamatwa.

Viongozi wa mandamano hayo wanasema kuwa kwa kuamrisha kutolewa kwa vizuizi, kiongozi wa Hong Kong CY leung ameweka vizuizi kwenye mazungumzo.