Ujerumani na mikakati dhidi ya Ebola

Haki miliki ya picha AP
Image caption Frank-Walter Steinmeier

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier anasema nguvu kubwa inahitajika dhidi ya kirusi cha ugonjwa wa Ebola.

Katika ufunguzi wa kikao cha Shirika la Afya Dunia mjini Berlin Ujerumani maongezi yaliyotawa ni kuhusiana na janga la Ebola

Steinmeier anasema wataalamu wa dawa na vifaa vingi vinahitajika ili kutoa msaada katika nchini tatu zinazo angamia kwa janga la Ebola Magharibi mwa Afrika.

Bwana Steinmeier ameahidi kutoa misaada na vikosi vingi kutoka Ujerumani kusaidia kupambana na janga hilo.

Mawazo ya Waziri wa Ujerumani yalitolewa baada ya Rais wa Liberia kuomba msaada nchi zote duniani Kusaidia kupambana na virusi vya Ebola.

Rais Ellen Johnson Sirleaf anasema kizazi chote cha vijana wa Afrika kiko hatarini kwa sababu ya maafa ya kiuchumi yanayosababishwa na ugonjwa huo.