Wanaume watano wauwawa Moyale, Kenya

Al Shabaab

Ripoti kutoka Kenya zinasema kuwa askari wa usalama wamewauwa watu watano wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa kundi la wapiganaji Waislamu wa Somalia, Al-Shabab, ambao wakijitayarisha kufanya mashambulio ya kujitolea mhanga.

Vyombo vya habari vya Kenya vinaeleza kuwa wanaume watano waliuliwa Jumamosi katika mji wa Moyale ulioko mpakani, wakati watu hao wakijaribu kuvuka mpaka na kuingia Kenya kutoka Ethiopia.

Msemaji wa ulinzi, (Bogita Ongeri) ananukuliwa akisema kuwa kilo 100 za mabomu na fulana 6 za kuficha mabomu ya kuripua wakati wa kujitolea mhanga, zilikutikana katika gari lao.

Msemaji wa ulinzi alieleza kuwa watu hao waliwafyatulia risasi askari wa usalama ambao walijibiza kwa kuwapiga risasi na kuwauwa.