Andy Murray ambwaga David Ferre

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Andy Murray

Mchezaji Tennis Andy Murray amembwaga David Ferrer katika mashindano ya wazi ya Vienna kwa seti

5-7 6-2 7-5. Kwa ushindi huo Andy Murray anasonga mbele katika mashindano hayo kwaajili ya kufuzu kuingia katika fainali za dunia.

Murray mwenye umri wa miaka 27 hii inakuwa mara tatu kumshinda mpinzani wake huyo katika hatua ya kuwania fainal.

Hata hivyo Murray muda mfupi baada ya mchezo huyo aliiambia BBC Radio 5 kwamba alikuwa amemaliza wiki yake vizuri katika mchezo huo uliomalizika baada ya saa mbili na dakika 42.

Ameongeza kuwa mchezo huo ulikuwa mgumu kwake ukizingatia umhimu wake katika kufuzu kuelekea fainali za London.