Ebola:Rais wa Liberia aomba ushirikiano

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Ellen Sirleaf Johnson

Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ametoa wito kwa nchi zote duniani kusadia kupambana na ugonjwa wa Ebola.

Kupitia barua kwa kipindi cha BBC cha (wikendi) Bi Sirleaf amesema kuwa dunia yote ina jukumu katika vita hivyo kwa kuwa ugojwa wa ebola hautambui mipaka.

Amesena kuwa ebola imefanikiwa kuvuruga taifa la Liberia ambapo umewaua zaidi ya watu 2000 katika kipindi cha miezi sita.

Siku ya Jumamosi rais wa zamani wa Cuba Fidel Castro alisema kuwa nchi yake itatuma madaktari 300 zaidi pamoja na wauguzi kusadia kupambana na ugonjwa wa ebola Magharibi mwa Afrika.

Cuba tayari imetuma madaktari 165 na wauguzi kwenda Afrika Magharibi.