Wanajeshi saba wauawa na bomu Misri

Haki miliki ya picha AP
Image caption mlipuko

Maafisa nchini Misri wanasema kuwa takriban wanajeshi saba wameuawa na wengine wanne kujeruhiwa baada ya bomu lililokuwa limetegwa kando kando ya barabara kulipuka katika mkoa wa Sinai.

Mlipuko huo ulilikumba gari lao ambalo lilikuwa likipiga doria katika eneo ambalo bomba la gesi linapitia katika mfereji.

Kumekuwa na mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya jeshi la Misri pamoja na miundo msingi katika eneo la Sinai tangu rais Abdel fatah al Sisi achukue uongozi wa taifa hilo mwaka 2013.