AFCON ya wanawake yafika ukingoni

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption AFCON

Michuano ya fainali za 9 za kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake imeingia hatua ya nusu fainali huko Namibia.

Mabingwa mara sita wa kombe hilo Nigeria wamepangwa kumenyana na Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza utakaopigwa kesho jumatano jioni kwenye dimba la Sam Nujoma jijini Windhoek.

Mchezo wa pili utaungurumishwa kwenye uwanja huo huo baadaye usiku kati ya wababe Cameroun na Ivory Coast

Timu tatu zitawakilisha bara la Afrika katika fainali za kombe la dunia zitakazofanyika mwaka ujao nchini Canada. Kwa hali hiyo timu mbili zitakazocheza fainali pamoja na ile itakayoshika nafasi ya tatu ndiyo zitakazo cheza kombe la dunia.