Manowari zaitisha Sweden

Image caption Meli

Jeshi la Maji la Sweden limesonga mbele zaidi katika eneo la maji la mji wake wa Stockholm katika hali ya kuendelea kuitafuta inayo kisiwa kuwa manowari kutoka urusi.

Jeshi limevitaka vyombo vyote vya kiraia kusogea mbali na eneo kati ya kisiwa cha Natttaro na Danziger Gatt.

Chanzo katika Sweden kimeiambia BBC kuwa chombo cha chini ya maji kimeonekana katika eneo la maji karibia kilomita 25 au maili 16 kutoka Stockholm

Waziri wa ulinzi wa Urusi amekataa nchi yake kuhusishwa kwa namna yoyote.

Baadaye Manowari hiyo ilisemwa kuwa huenda imetokea Uholanzi ingawa wizara ya Ulinzi ya Uholanzi haraka imejitokeza na kukanusha tetesi hizo.

“Kwa vyovyote vile haikuwa manowari ya Uholanzi” Msemaji wa wizara akiwa Hague aliiambia BBC.

Ni takribani siku nne kuelekea ya tano tangu kuanza kwa msako unaohusisha meli na helikopita ili kukitafuta chombo hicho kilichoonekana katika eneo la maji la Sweden.

Hapo awali jeshi la Sweden lilisema lilikuwa likifuatilia matukio yanayoendelea baharini na likakanusha kuisaka Manowari.

Lakini pia jeshi hilo limeonyesha picha ya kitu baharini karibu na Stockholm ingawa picha haikuwa wazi sana kuweza kuona kitu hicho ni nini.