Mhariri wa Washington Post afariki

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ben Bradlee

Mhariri wa zamani wa gazeti la Washington Post Ben Bradlee aliyeongoza uhariri wa kashfa ya Watergate miaka ya 70 na iliyosababisha Rais Richard Nixon kuachia ngazi amefariki akiwa na miaka 93.

Ben aliwahamasisha waandishi wawili wa habari Bob Woodward na Carl Bernstein kufuatilia kashfa hiyo ambayo Rais pia alijikuta akihusika.

Habari iliyochapishwa na gazeti hilo baadae ilionekana pia katika filamu na hivyo kumpa umaarufu mkubwa sana mwandishi huyu nguli.

Ben Bradlee hadi anakumbwa na mauti amekuwa ni miongoni mwa watu wanaohesabika kufanya kazi zenye tunu na hasa uadilifu aliouonyesha, Bwana alitoa na sasa amtwaa Amen.