Mwakilishi wa Kenya nje ya Big Brother

Image caption Sabina alikuwa anamkosa sana mwanawe alipokuwa ndani ya nyumba ya Big Brother

Baada tu ya wiki mbili katika nyumba ya Big Brother Mwakilishi mmoja wa Kenya Sabina ametimuliwa.

Sabina ana mtoto wa miezi minane na ndio mkenya wa kwanza kutimuliwa kutoka katika nyumba hiyo.

Inadaiwa kuwa watazamaji na mashabiki wa makala hiyo waliamua kumuondoa Sabina baada ya siku 14 pekee ili aende kumuhudumia mwanawe.

Sabina alionekana kumkosa sana mwanawe na wakati mwingi alionekana akifunga vitu kwenye mgongo wake ungedhani anambeba mtoto.

Image caption Sabina alionekana kuwa kipenzi cha wengi

Aliweka pamoja blanketi na nguo na kuvifunga kwenye mgo wake akiwa na kofia ya mwanawe huku akitembea katika nyumba hiyo kabla ya kujiunga na wenzake waliokuwa wakijivinjari nje.

Baadhi wanasema kufunga vitu mgongoni ndio chanzo za mashabiki kuanza kuomuonea huruma Sabina wakisema bora aende nyumbani kwa mwanawe mwenye miezi minane.

Na hapo ndipo walipompigia kura Jumapili na kumtimua kutoka katika Big Brother house.

Sabina alitimuliwa kutoka katika nyumba hiyo pamoja na Lilian kutoka Nigeria na Esther wa Uganda.

Hatua ya kumondoa Sabina katika Big Brother house inamwacha mwakili mmoj tu wa Kenya Melvin Alusa ambaye ni kakake Ben aime Baraza wa kikundi cha wanamuziki cha Sauti Sol.