Pistorius kutoshiriki mashindano

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Oscar Pistorious

Kamati ya Olimpiki ya Walemavu imesema mwanariadha Oscar Pistorius hata kama atatoka Gerezani kabla ya miaka mitano marufuku kushiriki katika mashindano ya riadha kwa walemavu itakayofanyika Rio mwaka 2019.

Hata hivyo haijafahamika wazi iwapo anaweza kuruhusiwa kushiriki katika mashindano ya wasio walemavu wakati akitumikia adhabu yake. Kamati hiyo imeongeza kuwa Oscar anaweza kushiriki katika mashindano yatakayofanyika Tokyo mwaka 2020. Utakumbuka kuwa Oscar Pistorius alikuwa mwanariadha mlemavu wa kwanza kushiriki katika Olympic isiyo ya walemavu iliyofanyika jijini London mwaka 2012. Jaji Thokozile Masipa amemuhukumu Pistorius miaka mitano jela kwa kosa la kumuua bila kukusudia mpenziwe mwanamitindo Reeva Steenkamp.