'Busu' lamtia mashakani Obama

Image caption Obama akibusu Cooper

Rais wa Marekani, Barack Obama, ametoa kauli yake kuhusu mwanamume aliyeshikwa na wivu baada ya yeye kumbusu mpenzi wake kwenye mashavu.

"rais tafadhali usimguse mpenzi wangu," alisema mwanamume, aliyetambuliwa na CNN kama Mike Jones.

Yote hayo yalitokea wakati Obama alipokuwa anapiga kura ya mapema katika jimbo la Illinois karibu na mwanamke aliyetajwa tu kama Aia Cooper.

''Kusema kweli sikuwa nimepanga kufanya hivyo,'' alisema Rais Obama , huku akiendelea kupiga kura yake huku Copper akiangua kicheko.

Baadaye Copper aliyeonekana kushikwa na aibu aliomba radhi kwa niaba ya mpenzi wake.

Obama alionekana naye kashikwa na aibu na kusema kwa tabasamu kuwa ,''hiki ni kisa tu cha mwanamume ndugu yangu kutaka tu kuniabisha bila sababu,''

Baada ya maongezi ya muda mfupi kati ya Obama na Cooper, wawili hao walimaliza kupiga kura, na kamera ikaonyesha Obama akimbusu Cooper mashavuni na kumpa mpenzi wa Coopper sababu nyingine ya kuongea.